Peter wa P-Square abadili tarehe ya kuzaliwa, ajitenga na pacha wake

Peter wa P-Square abadili tarehe ya kuzaliwa, ajitenga na pacha wake

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Peter Okoye maarufu kama Mr P, ametangaza rasmi kubadilisha tarehe yake ya kuzaliwa kutoka Novemba 18 kwenda Novemba 30, bila kutoa sababu za uamuzi huo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha jana Jumatatu, Aprili 20, 2026 kwenye akaunti yake rasmi ya X (Twitter), Mr P alisisitiza kuwa uamuzi huo ni wa kibinafsi na akawaomba mashabiki wake kuuheshimu.

“Nathibitisha rasmi kuwa Novemba 18 si tena siku yangu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa. Tafadhali mfahamu kuwa sitapokea ujumbe wowote wala zawadi siku hiyo. Siku yangu ya kuzaliwa sasa itasherehekewa Novemba 30. Huu ni uamuzi wa kibinafsi, na ninathamini sana uelewa wenu,”ameandika.

Hatua hiyo ina maana kuwa sasa Mr P hatasherehekea tena siku ya kuzaliwa pamoja na pacha wake, Paul Okoye maarufu kama Rudeboy, ambaye walizaliwa siku moja.

Hatua hiyo inaendelea kuongeza sintofahamu tangu kuvunjika kwa kundi la P-Square tangu 2016 ambapo lilikuwa linaundwa na mastaa hao ambao walitambana na ngoma kama ‘Chop My Money’, ‘Personally’, ‘No One Like U’ na nyingine nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button