Tiwa Savage Akanusha Kuhusiana na Don Jazzy
Tiwa Savage Akanusha Kuhusiana na Don Jazzy
Mwanamuziki wa Nigeria TiwaSavage,
amevunja ukimya kuhusu madai ya muda mrefu kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na DonJazzy, bosi wake wa zamani wa lebo ya Mavins.
Kwa mujibu wa RoyalBlog, Tiwa alieleza kuwa madai hayo hayana msingi wowote na alisisitiza kuwa uhusiano wao.ulikuwa wa kikazi tu. “Don Jazzy ni mtu mstaarabu sana
ambaye alihakikisha kila kitu kinafanyika kwa weledi” alisema Tiwa.
Akiendelea kueleza, Tiwa alikiri kwamba mara nyingi walifanya kazi usiku kucha wakiwa studio, na wakati mwingine alionekana akiwa amevaa mavazi yanayoweza kueleweka vibaya.
Hata hivyo, Don Jazzy alichukulia hilo
kwa utani na heshima, akimwambia, “Tiwa, tumeona haya yote, sio kitu kipya.”
Kwa kauli yake, Tiwa amefuta dhana potofu na kuwahakikishia mashabiki kuwa ushirikiano wake na Don Jazzy ulikuwa wa kazi tu bila mchanganyiko wa masuala
ya kimapenzi.