Aenda Mahakamani Kisa Mke Kumnyima Unyumba

Aenda Mahakamani Kisa Mke Kumyima Unyumba

Mwanaume kutoka Harare,JosephKatumba, amemshutumu mkewe,StellaKangara, kwa kumnyima haki zake za ndoa kwa karibu muongo mzima kama adhabu kwa kuwa hana ajira.

Katumba alishiriki mateso yake mahakamani akidai kuwa mkewe humkataa kwa vurugu kila anapojaribu kuomba tendo la ndoa.

“Anapiga kelele, ananionesha meno na kunikwaruza kila ninapomgusa. Anapiga kelele, Unataka kuniua!” -Alisema mahakamani.

Akielezea jinsi alivyokuwa akilala chini kwa miaka tisa huku mkewe akilala kwenye kitanda cha ndo Katumba aliomba amri ya ulinzi dhidi ya mkewe akidai vitendo vyake vilikuwa ni unyanyasaji wa kihisia na kisaikolojia.

Katika kujitetea, Stella alieleza kuwa kutokuwa na kazi kwa mumewe kumemfanya asionekane kuwa wa kuvutia.

“‘Sio chombo cha ngono. Nahitaji usalama wa kihisia na kifedha ili nijihisi kupendwa na kuthaminiwa. Kutokuwepo kwa jitihada za mume wangu kutafuta kazi kumekatisha tamaa yangu ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wakati mwingine tunalala tumekosa chakula, halafu anahitaji ngono wakati mimi sina nguvu hata kwa hiyo,” alieleza mbele ya mahakama.

Hakimu Meenal Naratom, aliyeongoza kesi hiyo, alikemea vitendo vya Stella, akisisitiza kuwa ukosefu wa ajira, ingawa ni changamoto kubwa, hauwezi kuwa sababu ya kuhalalisha unyanyasaji wa kimwili na kihisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button