Tuzo za Oscar Kufanyika Kama Kawaida Licha ya Moto wa Los Angeles
Tuzo za Oscar Kufanyika Kama Kawaida Licha ya Moto wa Los Angeles
Tuzo za Oscars zitaendelea kama ilivyopangwa tarehe 2 Machi licha ya hali ya sasa ya moto huko Los Angeles.
Moto wa Palisades na Eaton, ambao kwa pamoja umeharibu zaidi ya ekari 37,000, bado unaendelea kuwaka.
Hata hivyo, Academy imetangaza kuwa hafla hiyo itaendelea kama ilivyopangwa.
“Tumechukua uamuzi wa kufikiria kwa makini kuendelea na hafla ya 97 ya Oscars kama ilivyopangwa tarehe 2 Machi’ alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Academy, Bill Kramer, katika taarifa yake.
“Hafla ya mwaka huu itajumuisha nyakati maalum kutambua wale waliojitoa kwa ujasiri kupambana na moto huu.
Hii ndiyo sababu hasa tunahisi tunapaswa kuendelea mbele – kutumia jukwaa letu la kimataifa kuleta uelewa juu ya matukio haya muhimu katika historia yetu,”
“Roho ya Los Angeles daima imekuwa ya uvumilivu, na Oscars siyo tu sherehe ya filamu, bali pia ni sherehe ya nguvu na mshikamano wa jamii yetu wakati wa changamoto” taarifa hiyo ilihitimisha.