Rais Wa Bukinafaso Akataa Kuongezewa Mshahara.
Rais wa Bukinafaso Akataa Kuongezewa Mshahara
Rais wa Burkina Faso, Kapteni IbrahimTraoré, mwenye umri wa miaka 37, amekataa ongezeko lolote la mshahara, akisisitiza kujitolea kwake kwa wananchi wa nchi hiyo.
Traoré, ambaye alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi, alitangaza kuwa utajiri wake wote ni shilingi milioni 340 za Kitanzania na ataendelea kupokea mshahara wake wa kawaida kama kapteni wa jeshi.
Uamuzi wake wa kukataa ongezeko la mshahara ni tofauti kubwa na hatua za baadhi ya watangulizi wake, ikiashiria enzi mpya ya uongozi.