Lori Lagonga Kituo Cha Mwendokasi Barabara Ya Nyerere.
Lori Lagonga Kituo Cha Mwendokasi Barabara ya Nyerere
Lori limegonga kituo cha mwendokasi
kilichopo Barabara ya Nyerere upande wa kutokea Gongo la Mboto kuelekea mjini leo Machi 25, 2025 baada ya kuacha njia na kushindwa kuendelea kwenye njia ya
magari ya kawaida.
Jitihada za uokoaji zinaendelea ambapo wasamaria wema wanadai kuwa bado dereva wa lori hilo amenasa kwa ndani kutokana na kubanwa na vyuma vya kituo
hicho.