Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Yasonga Mbele na Miradi ya Maendeleo ya Kidijitali

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.) ameyataja mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya Mawasiliano katika mwaka wa fedha 2024/2025 kuwa ni pamoja na kusainiwa kwa mkataba wa kukabidhi miundombinu ya Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano kwa Serikali, ambapo kilometa 336 kati ya 2,020 zimekabidhiwa.

Akizungumza leo Machi 24, 2025 wakati akiwasilisha utekelezaji wa Mpango wa Bajeti wa 2024/25 na makadirio ya 2025/26 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bungeni jijini Dodoma, amesema Wizara hiyo pia imefanikiwa kusaini mkataba wa fedha na Benki ya Exim ya China kwa ajili ya ujenzi wa minara 636.

Kwa upande wa usalama mtandaoni, amesema Wizara imezindua kampeni ya SITAPELIKI ili kupambana na utapeli na ulaghai wa mtandaoni, huku Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikifanikiwa kutoa leseni 939 kwa watoa huduma mbalimbali za mawasiliano, zikiwemo leseni 456 za rasilimali namba na leseni 48 kubwa.

Katika usimamizi wa vifaa vya kielektroniki, TCRA ilikagua vifaa 578 kati ya Julai 2024 na Februari 2025, ambapo vifaa 455 vilikidhi vigezo na kuidhinishwa. Pia, mamlaka hiyo ilifungia laini 37,983 za simu zilizohusika katika uhalifu mtandaoni.

Kwa upande wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kilometa 3,621 zimejengwa, sawa na asilimia 82 ya lengo la kilometa 4,442, huku vituo 111 vya huduma za Mkongo vikikamilika kwa asilimia 100, sambamba na kukamilisha taratibu za manunuzi ya ujenzi wa kilometa 186 za Mkongo wa Taifa kutoka Kigoma hadi Kalemie (DRC) hatua inayolenga kuimarisha mawasiliano ya kikanda kupitia Ziwa Tanganyika.

Aidha, Serikali inajenga minara 758 katika kata 713, ambapo hadi Februari 2025, jumla ya minara 443 imejengwa na minara 417 kati ya hiyo inatoa huduma za mawasiliano.Katika kuboresha upatikanaji wa intaneti, minara 304 iliyokuwepo imeboreshwa kutoka 2G hadi 3G/4G.

Wizara pia imekamilisha uhakiki wa Anwani za Makazi katika Halmashauri 41, huku mifumo 13 ya utoaji huduma ikiunganishwa na mfumo wa NaPA. Taarifa za anwani za makazi pia zimekusanywa

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button