Jay-Z na P Diddy Hawana Uhusiano Wowote Nje ya Kazi

Jay-Z na P Diddy Hawana Uhusiano Wowote Nje ya Kazi

Katikati ya kesi inayoendelea ya madai ya
ubakaji dhidi ya Jay-Z na Sean “Diddy” Combs, wakili wa Jay-Z, Alex Spiro, ametoa ufafanuzi kuhusu uhusiano kati
ya wasanii hao wawili.

“Bw. Carter hana uhusiano wowote na kesi ya Bw. Combs au Bw. Combs mwenyewe,” alisema Spiro. “Walijuana kikazi kwa miaka kadhaa. Kama ilivyo kwenye taaluma
nyingine, watu wanajuana.

Wanapokutana kwenye tuzo za muziki, wanasaidiana. Wanaenda kwenye mechi za
NBA AIl-Star, wanasaidiana. Hivyo ndivyo taaluma zinavyofanya kazi”

Spiro alikanusha madai ya uhusiano wa karibu zaidi kati ya wawili hao, akiyaita hadithi za kubuni, na kusisitiza
kuwa Jay-Z hana uhusiano wowote na mashtaka au madai yanayomkabili Diddy.

“Hana uhusiano wowote na kesi hiyo na hakuna kingine cha kusema” alihitimisha
Spiro.

Wote wawili wanakabiliwa na madai yanayohusiana tukio linalodaiwa kutokea mwaka 2000, ingawa Jay-Z amekanusha madai hayo vikali, akiyaita yasiyo na msingi
na yanayochochevwa na tamaa ya fedha na umaarufu.Kesi inaendelea huku pande zote zikiwasilisha hoja zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button