Diamond Platnumz Aongoza Kutazamwa Kenya 2024
Diamond Platnumz Aongoza Kutazamwa Kenya 2024
Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwana Nairobi Gossip Club, @Diamond Platnumz ameongoza kama msanii aliyetazamwa zaidi kwenye YouTube nchini Kenya mwaka 2024, akikusanya jumla ya watazamaji milioni 125.
Hakuna shaka kwamba Diamond ameendelea kuthibitisha ubabe wake kwenye soko la Afrika Mashariki.
Harmonize_tz na Rayvanny wanashikilia nafasi ya pili na ya tatu kwa watazamaji milioni 85.6 na milioni 83.4.
Wakati huo huo, @lsraelMbonyi kutoka Rwanda ameonyesha umaarufu wake kwa kushikilia nafasi ya nne akiwa na watazamaji milioni 75.4.
Kwa upande wa wasanii wa kike OfficialZuchu ameendelea kuwa kipenzi cha wengi, akiwa nafasi ya tano na watazamaji milioni 73.6. Mbosso naye, kutoka WCB_VWasafi, ameshikilia nafasi ya sita na watazamaji milioni 56.1, akionyesha jinsi Bongo Fleva inavyozidi kuvutia mashabiki wa muziki Kenya.
Orodha hii pia imejumuisha wasanii kutoka Nigeria, kama Ayra Starr aliye nafasi ya kumi na Chris Brown kutoka Marekani, wakithibitisha jinsi muziki wa kimataifa unavyopokelewa vizuri Kenya.