Kendrick Lamar Hakulipwa Kwenye Show Ya Super Bowl 2025.

Kendrick Lamar Hakulipwa Kwenye Show ya Super Bowl 2025

Mshindi wa Tuzo za Grammy na msanii
maarufu wa hip-hop kutoka Los Angeles, Kendrick Lam aliongoza shoo ya mapumziko ya Super Bowl LIX Jumapili, akitumbuiza mbele ya watazamaji zaidi ya milioni 120.

Shoo hiyo, ambayo ilidumu kwa dakika 13,
ilijumuisha wimbo wake maarufu wa kumkashifu Drake, Not Like Us, ambao ulishinda kwenye vipengele vyote tano alivyoteuliwa kwenye Tuzo za Grammy wiki
iliyopita.


Ingawa shoo hiyo itakuwa mnoja ya majukwaa makubwa zaidi ya mwaka kwa KendrickLamar, inaweza kushangaza mashabiki wake kujua kwamba msanii huyo
mwenye miaka 37 hatalipwa senti moja kwa ajili ya kuburudisha stejini hapo.

Shirika la National Football League (NFL) halilipi wasanii kwa kuimba katika shoo ya
mapumziko ya Super Bowl, ingawa linatoa fedha kwa gharama za utayarishaji na uzalishaji wa maudhui ya tukio
hilo.

Kwa kawaida, wasanii wanaokubali mwaliko wa Super Bowl hufanya hivyo kwa sababu za kimaarufu na kupata pesa kwa njia zingine.

Kuwepo kwenye jukwaa hilo inawapatia umaarufu mkubwa, kuongezeka kwa mauzo
ya nyimbo, na fursa za kibiashara.

Kwa Kendrick Lamar, shoo hii ilikuwa fursa ya kujitangaza kwa watazamaji wengi na kuimarisha nafasi yake kama moja ya wasanii bora wa hip-hop wa kizazi chake.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki waligawanyika kuhusu shoo yake, wakati wengine walipendezwa na ubunifu wake na uhalisi, wengine waliona haikufikia matarajio yao.

 

Lakini bila shaka, kuvuma kwa NotLikeUs na ushindi wake wa Grammy zitaongeza mwaka wa umaarufu wake.

Kwa hivyo, ingawa Kendrick Lamar hatalipwa moja kwa moja kwa kutumbuiza Super Bowl, faida za kimaarufu na kifedha zinazotokana na tamasha hilo zinaweza kuwa na thamani kubwa zaidi kuliko malipo ya moja kwa moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button