Aliyepinga Rais Samia Kupitishwa Mgombea Pekee Urais CCM Afukuzwa.

Aliyepinga Rais Samia Kupitishwa Mgombea Pekee Urais Afukuzwa CCM

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho.

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuvwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button