Kanye West Ataja List Ya Watu Waliowahi Kumsaliti.
Kanye West Ataja List Ya Watu Waliowahi Kumsaliti.
Rapa na mfanyabiashara KanyeWest ametaja orodha ndefu ya watu na taasisi ambazo anadai zimemsaliti.
Kupitia maandīko yake, Kanye alieleza kuwa ana maumivu ambayo hakuna mtu anayeweza kuyatibu.
Orodha yake inajumuisha marafiki wa karibu, wasanii wenzake, akiwemo Jay-Z, Pusha T,Ty Dolla $ign na wengine.
Kwa miaka mingi, Kanye amekuwa na mahusiano ya karibu na baadhi ya watu hawa, lakini tofauti na migogoro ya muda imewafanya kutengana.
John Legend na Big Sean, walikuwa sehemu ya familia yake ya kisanii kupitia label yake ya GOODMusic, lakini baadaye walijitenga naye.
Kid Cudi, rafki wa muda mrefu, pia alitofautiana naye baada ya Kanye kumkosoa kwa urafiki wake na Pete Davidson.
Kim Kardashian, aliyekuwa mke wake, anatajwa na Ye kila siku ikionyesha bado kuna mgawanyiko mkubwa kati yao licha ya kuwa na watoto pamoja. The Kardashians, kwa ujumla, wanaonekana kuwa sehemu ya watu anaowahisi kama waliomsaliti, jambo ambalo linaweza kuhusiana na mgogoro wa ndoa na talaka yake.
Kwa upande wa biashara, Kanye aliwataja Adidas na Balenciaga, makampuni aliyowahi kushirikiana nayo lakini baadaye yakamtema baada ya matamshi yake tata kuhusu Wayahudi. Demna, mbunifu mkuu wa Balenciaga, pia alitajwa, ikionesha kuwa Kanye ana hisia kali kuhusu kuvunjika kwa ushirikiano wao.
Kilichoshangaza wengi ni Kanye kuwataja watoto wake na familia yake mwenyewe, pamoja na Jumuiya ya Watu Weusi na Wayahudi, akionesha hisia za kukosa msaada kutoka kwa jamii nzima.
Ujumbe wake unaonesha maumivu na huzuni aliyonayo, lakini pia unaibua maswali kuhusu hali yake ya kiakili na hisia zake kuhusu watu waliokuwa karibu naye.
Je, hii ni njia ya Kanye kuonesha hisia zake, au ni mwanzo wa drama nyingine kubwa kwenye maisha yake?