Mwanafunzi wa Kidato Cha Pili Abakwa Ofisini Kwa Mwalimu Mkuu
Mwanafunzi wa Kidato Cha Pili Abakwa Ofisini Kwa Mwalimu Mkuu.
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Zombo iliyopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumbaka
Mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro SACP. Alex Mkama amemtaja Mwalimu huyo anayetuhumiwa kubaka kuwa ni Mkame Mwaisumo (30) na kwamba anadaiwa kufanya kosa hilo majira ya asubuhi March 19, 2025 ndani ya Ofisi ya Mwalimu Mkuu baada ya kumtuma akachukue andalio
la somo.
RPC Mkama amesema baada Mwanafunzi huyo kwenda ofisi aliyokuwa amemtuma, Mwalimu alimfuata ndani na kumfanyia ukatili huo.
Amesema Mwalimu huyo alikuwa ana kaimu nafasi ya Mkuu wa Shule na uchunguzi wa awali umebaini chanzoni mmomonyoko wa kimaadili Kwa Mwalimu huyo, kwa sasa Mwalimu anaendelea kuhojiwa na upelelezi
utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.