Raia Wa Tanzania Sasa Mtaingia Congo Bila Viza.
Raia Wa Tanzania Sasa Mtaingia Congo Bila Viza.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kwamba, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)nimeondoa hitajio la visa kwa Raia wa Tanzania
wanaoingia DRC kuanzia March 20, 2025.
Taarifa iliyotolewa na Wizara imesema baada ya Jamhurinya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kujiunga na Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) mwezi July 2022 baadaye September 02, 2023, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliondoa utaratibu wa malipo ya visa kwa raia wa
DRC kwa matarajio ya nchi ya DRC pia kufuta utaratibu wa kutoza malipo ya visa kwa msingi wa kuungana mkono (reciprocity).
Serikali ya Jamhuri wa Tanzania inaamini kuwa uamuzi huu wa Serikali ya DRC ni hatua nzuri katika kuimarisha mtangamano na utakuwa na manufaa, ikizingatiwa kuna
mwingiliano mkubwa wa Wananchi wa nchi hizi mbili katika masuala mbalimbali ya kijamii na kibiashara,nvilevile kuondolewa kwa hitajio la visa kutachochea ukuaji
wa uwekezaji, biashara na kupunguza gharama.
“Hatua hii ni moja ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuimarisha
mahusiano ya kidiplomasia na ujirani mwema kwa vitendo, na ni ishara ya Tanzania kuzingatia miongozi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, pamoja na Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA)”