Ahukumiwa Kunyongwa Mpaka Kufa kwa Kosa La Kuuwa.

Ahukumiwa Kunyongwa Mpaka Kufa kwa Kosa La Kuuwa.

Mahakama ya Mkoa wa Singida imemhukumu Charles Joseph Mwandu (63), mkulima na mkazi wa Kijiji cha lyumbu, Wilaya ya Ikungi, adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la mauaji.

Mwandu alitenda kosa hilo Novemba 1, 2024, katika Kijiji cha Iyumbu, Tarafa ya Sepuka, kwa kumkata Mwambula Mumbi sehemu mbalimbali za mwili kwa kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha yaliyosababisha kifo. Alikamatwa na kufikishwa Mahakamani Novemba 29, 2024.

Hukumu hiyo imetolewa Januari 8, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa Allu Mzowa, baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button