Inawezekana Kuishi Bila Upendo lla Sio Bila Maji.

Inawezekana Kuishi Bila Upendo lla Sio Bila Maji.

Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza hafla ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya maji ya mwaka 2002 toleo la mwaka 2025 iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Katika hotuba yake Rais Samia amesisitiza kuwa maji si rasilimali ya kawaida bali ni uhai, uchumi na msingi wa utulivu wa Jamii akifananisha umuhimu wake na Viongozi bora wanaohudumia Wananchi bila ubaguzi

“Kazi ya maji kwanza ni kuleta uhai, unaweza kuishi bila upendo lakini hauwezi kuishi bila maji, unaishi Watu kadhaa wanakuchukia lakini si unaishi bwana, au chukiwa na Watu wote kama Mungu anataka kukupa uhai utaishi lakini kuwe hakuna maji niambie unaishije!?”

“Kama hakuna maji hakuna chakula, hakuna dawa, maji yanatusaidia viwandani kuzalisha mambo mbalimbali, ndio maana Wawekezaji wanauliza unanipa site kuna.umeme na maji? kama hamna siendi huko nipe kwingine, bila maji pia hakuna ajira, hakuna nishati, bila maji hakuna bwawa la Nyerere n.k

‘Maji ni utulivu wa nchi, katika makala mliona kuna sehemu maji hamna Watu wamemkasirikia Waziri, maeneo yenye shida ya maji muweke foleni mmoja atoe madumu hapo patakalika?, kwahiyo maji yanasaidia utulivu wa kisiasa n.k, maji ni uchumi, ustawi wa jamii maji ni usalama wa Taifa, bila maji hakuna Taifa”

‘Maji yanafananishwa na Viongozi wazuri hapa Duniani, wanasema Viongozi huwa kama maji, husafishe wote bila kusema huyu hakunipa kura, huyu alinitukana, huyu alinisema vibaya, Kiongozi mzuri anahudumia Watu wote bila nongwa na hiyo ndio sifa ya maji hata kama jana uliyachafua ukienda yatakusafsha” Rais Samia akiongea kwenye uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 Toleo la mwaka 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button