Takribani Watu 9000 Hufariki Wanapojaribu Kuhamia Mataifa Mengine.
Takribani Watu 9000 Hufariki Wanapojaribu Kuhamia Mataifa Mengine
Karibu watu 9,000 wamepoteza maisha duniani kote katika njia za uhamiaji mwaka 2024. Vifo hivyo vinatajwa kuufanya mwaka 2024 kuwa mbaya zaidi kwa wahamiaji, Umoja wa Mataifa umesema mwishoni mwa juma huku ukiita ‘janga lisilokubalika na
linalozuilika’.
“Angalau watu 8,938 walifariki katika njia za uhamiaji duniani kote mwaka 2024. “Huu ni mwaka wa tano ambapo idadi imefikia kiwango cha juu zaidi,” Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM) lilieleza.
Naibu Mkurugenzi wa IOM, Ugochi Daniels amesema Janga la kuongezeka kwa idadi ya vifo vya wahamiaji duniani kote halikubaliki na linazuilika, Daniels amesema wanaopotea ni binadamu na kupotea kwao ni janga. “Idadi halisi ya vifo na kutoweka kwa
wahamiaji kuna uwezekano mkubwa wengi
hawajaandikwa kwa sababu ya uhaba wa vyanzo rasmi,”
Asia, Afrika na Ulaya zilikuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wanaokufa ambapo kwa mwaka 2024 pekee walifariki wahamiaji 5253 mtawalia.