50 Cent Amchokoza Jay Z na Kesi ya Ubakaji.
50 Cent Amchokoza Jay Z na Kesi ya Ubakaji.
Rapa 50 Cent, anayejulikana kwa utanii
wake wa mara kwa mara, amemchokoza Jay-Z kufuatia kuhudhuria kwake kwenye uzinduzi wa filamu ‘MufasaThe Lion King’ pamoja na mkewe BeyoncĂ© na binti yao
Blue lvy, huku akihusishwa na tuhuma za ubakaji wa msichana wa miaka 13.
Kupitia chapisho la lnstagram lililofutwa baadaye, 50 Cent aliandika, “Jay alisema wamesema nimembaka mtoto, kila mtu vaeni nguo tunaenda kwenye uzinduzi wa
Mufasa LOL” akiambatanisha picha ya familia ya Carter kwenye zulia jekundu.
Jay-Z, Beyoncé, na mama mkwe wake Tina Knowles walihudhuria tukio hilo kumuunga mkono Blue lvy, aliyetoa sauti ya Princess Kiara katika prequel ya *The Lion King*.

Hii ilitokea siku moja baada ya Jay-Z kutajwa katika kesi ya madai, ambapo anatuhumiwa, pamoja na Sean “Diddy” Combs, kumbaka msichana huyo mwaka 2000.
Jay-Z alikanusha vikali tuhuma hizo, akieleza kuwa ni njama ya kisheria dhidi yake, na kuomba mwathiriwa ashtaki kwa kesi ya jinai badala ya madai.





