Chadema yahoji mamilioni yake kuzuiwa, Ofisi ya Waziri Mkuu yaeleza

Chadema yahoji mamilioni yake kuzuiwa, Ofisi ya Waziri Mkuu yaeleza

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuingilia kati suala la kuzuiwa kwa fedha za ruzuku za chama hicho kiasi cha Sh500 milioni na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kinyume na kisheria.

Amesema fedha hizo ni halali kwa Chadema na zinahusu kipindi cha Juni hadi Oktoba 2025. Fedha hizo zinatokana na uwakilishi wa chama hicho bungeni. Huku akieleza wasiwasi wao ni kuwa fedha hizo zinaweza kurejeshwa Hazina kutokana na mwaka wa fedha wa Serikali kuelekea ukingoni.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dk Jim Yonazi, ambaye katika majibu yake amejitenga na suala hilo akidai lipo chini ya mamlaka ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Kama wanadai fedha hizo, ni wajibu wao kutambua kuwa ofisi inayohusika ni Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na si Ofisi ya Waziri Mkuu kama wanavyodai, hatuwezi kuingilia,” amesema Dk Yonazi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumatano, Juni 17,2026 Mnyika amesema Chadema imekuwa ikidai fedha hizo kwa muda mrefu kupitia barua mbalimbali kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na kupitia mikutano ya hadhara, lakini hadi sasa hakujaingiziwa kwenye akaunti ya chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button