IGP WAMBURA AONGOZA MKUTANO WA KUPIMA UTENDAJI WA JESHI LA POLISI.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura, ameongoza Mkutano wa upimaji wa Utendaji Kazi wa Jeshi la Polisi (PRM uliofanyika Julai 27, 2026, katika Ukumbi wa Polisi Jamii,jijini Dodoma
Mkutano huo umewakutanisha Makamishna wote wa Jeshi la Polisi kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu na kuimarisha ufanisi wa utendaji ndani va Jeshi.
<atika kikao hicho, viongozi wa Jeshi la Polisi wamepokea na kujadil aarifa mbalimbali za utekelezaii wa maiukumu va Jeshi la Polisi,utekelezaj wa mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai pamoja na ufanya tathmini ya mafanikio yaliyopatikana na changamotc zilizojitokeza katika utekelezaji wa shughuli za Jeshi la Polisi. Aidha mkutano umejadili hatua za kuendelea kuboresha utendaji kwa kuzingatia vipaumbele vya taasisi.
Mkutano huo pia umethibitisha mipango na kuweka mikakati ya uendelea kulijenga Jeshi la Polisi la kisasa, lenye weledi na linalotoa huduma bora kwa jamii, sambamba na kuimarisha amani na usalama nchini kupitia utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi na uwajibikaji.
Miongoni mwa mambo yalivoendelea kutekelezwa na Jeshi la Polisi n pamoja na utekelezaji wa maelekezo va Tume va Haki Jinai kwa kuimarisha utoaji wa haki, uwajibikaj na ufanisi katika huduma za kipolisi, kuboresha taratibu za uchunguzi wa makosa ya jinai <uimarisha matumizi va teknolojia katika utendaji wa kazi na kuongeza nafunzo kwa askari kuhusu haki za binadamu na maadili va kazi.
Aidha, kuendelea kutolewa kwa elimu ya kubaini na kuzuia uhalifu kwa wananchi pamoja na kuimarishwa kwa ushirikiano kati va Jeshi la Polisi na taasisi nvingine za mfumo wa haki jinai ambao umeendelea <uimarishwa, jambo lililochangia kuharakisha utoaji wa haki na <uongeza imani ya wananchi kwa vyombo vya dola






