Barua Ya Wazi Ya Dula Makabila Kwa Diamond Plantnumz
Barua Ya Wazi Ya Dula Makabila Kwa Diamond Plantnumz
Msanii wa Dulla Makabila, amemshukuru Diamond Platnumz baada ya wawili hao kuwa karibu tena, akisema mwaliko wa kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Mama Dangote ulikuwa na maana kubwa kwake.
Dulla ameeleza kuwa Diamond amekuwa na mchango mkubwa katika maisha na muziki wake, akimtaja kuwa alimsaidia wakati wa changamoto za kifedha, akampa fursa mbalimbali na hata kugharamia sehemu kubwa ya sherehe ya ndoa yake ya kwanza. Amehitimisha kwa kusema kurejesha uhusiano wao ni ushindi mkubwa kwake.






