Dangote ” Maisha Yangu ni Ushuhuda Mungu Yupo”
Dangote "Maisha Yangu ni Ushuhuda Mungu Yupo"
Bilionea na Mfanyabiashara maarufu barani Afrika, Aliko Dangote amesema anaamini kwa asilimia 100 kuwa Mungu yupo, akieleza kuwa maisha na mafanikio yake binafsi yamempa ushahidi wa kutosha kuhusu uwepo wa Mungu.
Dangote ametoa kauli hiyo katika mahojiano na mtengeneza maudhui wa mtandaoni kupitia kipindi cha The School of Hard Knocks, baada ya kuulizwa iwapo anaamini Mungu yupo na ni nini kinachomfanya kuwa na imani hiyo.
Akijibu swali hilo, Dangote amesema imani yake haijajengwa na nadharia pekee bali pia na safari yake ya maisha na mafanikio aliyoyapata.
“Nikiangalia mimi mwenyewe, najua Mungu yupo,” amesema Bilionea Dangote.
Mbali na suala la imani, mahojiano hayo pia Dangote amezungumzia safari yake ya kujenga himaya kubwa ya biashara, utajiri pamoja na mtazamo wake kuhusu maisha na mafanikio.





