Mejakunta Afiwa na Baba Yake Mzazi

Mejakunta Afiwa na Baba Yake Mzazi

Baba Mzazi wa Msanii wa Bongo Fleva, Meja Kunta amefariki dunia leo Julai 21, 2026 katika Hospitali ya Temeke, Jijini Dar es salaam wakati akipatiwa matibabu huku chanzo kikitajwa ni presha.

Akizungumza na AyoTV kwa njia ya simu, Meneja wa msanii huyo, Waso Wiso amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kwamba wameanza taratibu za kimsiba.

“Mzee kaondoka, tumefika madaktari wametupa taarifa, shida ni strock na pressure,”

Msiba huo unakuja siku moja tu baada ya Meja Kunta kuomba msaada kwa kuuza baadhi ya mali zake ili kupata fedha za kuendelea kumtibia baba yake, akieleza kuwa tayari alikuwa ametumia fedha zake zote katika gharama za matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button