Sexyy Red Ashukuru Kwa Zawadi Ya Birkin “U My Everything”
Sexyy Red Ashukuru Kwa Zawadi Ya Birkin "U My Everything"
pulse_of_styles Rapa Drake amezidi kuonyesha ukarimu baada ya kumzawadia rapa mwenzake Sexyy Red mkoba wa kifahari wa Hermès Birkin. Wawili hao walikutana pamoja kuhudhuria fainali kubwa ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 jijini New York/New Jersey, tukio lililofatiwa na zawadi hiyo ya kipekee iliyoamsha msisimko mkubwa mtandaoni.
Zawadi hiyo ni mkoba wa rangi nyekundu iliyokolea wa Hermès Birkin 30 uliotengenezwa kwa ngozi inayong’aa ya mamba wa Porosus shiny Porosus crocodile leather. Thamani ya mkoba huo adimu katika masoko ya bidhaa za kishua inakadiriwa kuanzia dola $40,000 hadi $50,000.
Sexyy Red aliposti picha hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram akisindikiza na ujumbe uliosema: “Thanks for da Shabirkin baby daddy bae I love you. U my everything.” Kauli hiyo inagusia kwa ucheshi wimbo wao wa pamoja unaofahamika kama “U My Everything”. When Champagne Papi drops a $50k crocodile Birkin for the World Cup link up.






