Ibrahim Bacca Apandishwa Cheo Jeshini sasa ni Sajenti.
Ibrahim Bacca Apandishwa Cheo Jeshini Sasa ni Sajenti.
Beki wa Klabu ya Yanga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Ibrahim Hamad maarufu ‘Bacca’ amepandishwa cheo katika Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora uwanjani.
“Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), kimempandisha cheo mchezaji wetu lbrahim Hamad “Ibra Bacca” kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora uwanjani,”imeeleza taarifa hiyo iliyochapishwa leo Machi 17, 2025 katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Yanga