Ni Miaka Minne Tangu Dr.Magufuli Afariki Dunia

Ni Miaka Minne Tangu Dr.Magufuli Afariki Dunia.

Familia ya Rais awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ikiongozwa na Mjane wa Hayati Magufuli, Mama Janeth Magufuli, Viongozi mbalimbali na Watu wengine mbalimbali wameshiriki katika misa takatifu ya kumuombea Hayati Magufuli iliyofanyika Chato Mkoani Geita leo March 17,2025.

lbada hii imefanyika katika Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara Parokia ya Mt. Yohana Maria Muzeyi Mlimani na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Baba Askofu Severin Niwemgizi, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi, Ofsi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel.

Wengine walioshiriki misa hiyo ni pamoja na Mbunge wa Geita Medard Kalemani, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa, Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Rehema Sombi, Mtangazaji wa CloudsFM ambaye ni Mmiliki wa AyoTV Millard Ayo ambaye yupo kikazi Mkoani humo pamoja na Watu wengine mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button