Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina dhidi ya watumishi wa afya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), kufuatia tuhuma za rushwa na utoaji wa huduma usioridhisha.

Akizungumza katika kikao kilichohusisha uongozi wa uwanja huo, Bodi ya Utalii Tanzania, na watumishi husika, Desemba 28, 2024 Dkt. Mollel amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na kutotoa huduma kwa kufuata taratibu.
Katika kikao hicho ameagiza watumishi waliohusika kuchukuliwa hatua kali ikiwemo kusimamishwa kazi na wengine huhamishwa kituo cha kazi.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii alimwomba Naibu Waziri huyo kuwasamehe watumishi waliotuhumiwa na badala yake awape onyo kali ili waweze kurekebisha mienendo yao na kuzingatia weledi kazini.