Vazi la Mke wa Kanye West Lashangaza Grammy 2025
Vazi la Mke wa Kanye West Lashangaza Grammy 2025
BiancaCensori ameendelea kuthibitisha kuwa hana mipaka linapokuja suala la mitindo ya kuvaa, lakini safari hii alizua mshangao mkubwa alipohudhuria
Tuzo za Grammy akiwa nusu uchi kabisa. Mke wa KanyeWest huyo, mwenye umri wa miaka 30, alitembea kwenye zulia jekundu akiwa amevalia gauni jepesi lililoonyesha mwili wake wote wazi kabla avue koti lake na kufanya macho yote yamgeukie yeye.
Hali hiyo imezua mjadala mkali mtandaoni huku baadhi wakidai kuwa vazi lake linaweza kumwingiza matatizoni kisheria.
Sheria za California zinaeleza kuwa “kujitokeza uchi kwa makusudi mbele ya watu wanaoweza kukereka” kunaweza kuchukuliwa kama kosa la utovu wa maadili.
Baadhi ya mashabiki walitoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wengine wakidai kuwa Bianca alivuka mipaka.
Mmoja aliandika kwenye X (zamani Twitter): “Kanye huyo mwanamke wake wanapaswa kukamatwa kwa alichovaa kwenye Grammys.”
Huku Kanye West akiwa na tuzo mbili alizokuwa akiwania usiku huo, mjadala kuhusu mavazi ya Bianca unaonekana kuzidi kushika kasi mtandaoni.