Mtukufu Aga Khan IV Afariki Dunia Ureno
Mtukufu Aga Khan IV Afariki Dunia Ureno
Bilionea na Kiongozi Mkuu wa 49 wa
Madhehebu ya Shia lsmailia na Mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, Lisbon nchini
Ureno jana February 04,2025 na anatarajiwa kuzikwa Lisbon ingawa tarehe ya maziko bado haijawekwa wazi.
Shirika lake la misaada la Aga Khan Development Network limesema Mtukufu Aga Khan anayefahamika kama Karim A-Hussaini Aga Khan IV, amefariki akiwa
amezungukwa na Familia yake ambapo baada ya kifochake, Imamu wa 50 wa madhehebu ya Shia Ismailia atatangazwa kurithi mikoba ya Aga Khan IV.
Akiwa na umri wa miaka 20 alipewa wadhifa wa Aga Khan wa nne na Imamu wa 49 wa kizazi cha Ismailia October 19,1957 Jijini Dar es salaam Tanzania akimrithi Babu yake
Agha Khan Ill, enzi za uhai wake Mtukufu Aga Khan alifahamika kutokana na mchango wake kwenye shughulizi nazochangia kuimarisha ustawi wa maisha ya binadamu katika maeneo mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Afrika Mashariki.
Nchini Kenya na Tanzania Agha Khan ameacha alama isiyofutika kwa kuanzisha Taasisi mbalimbali zilizoleta mchango mkubwa katika maisha ya Raia wa Nchi hizi
mbili ambapo uwepo wa Aga Khan nchini Tanzania unaonekana kupitia uanzishwaji wa kampuni mbalimbali ikiwemo ya Mwananchi Communications Limited (MCL)Hospitali za Aga Khan na miradi mbalimbali katika sekta
ya afya na elimu.