Dkt. Jakaya Kikwete amewasilisha ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassankwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo – Brazzaville) Collinet Makosso Anatole

Ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan wapokelewa Congo-Brazzaville

Rais mstaafu na mjumbe maalumu wa Rais Samia Suluhu Hassan Dkt. Jakaya Kikwete amewasilisha ujumbe wa Rais kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Congo (Congo – Brazzaville) Collinet Makosso Anatole.

Ujumbe huo umepokelewa na Anatole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou Nguesso Jijini Brazzaville.

Dkt. kikwete pia amewasilisha salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button