Walioiba Kwenye Ajali Watupwa Jela.
Walioiba Kwenye Ajali Watupwa Jela.
Walinzi wawili Buhari Hassan na John Samson, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Zuba, Abuja, siku ya Jumanne, Aprili 1 5, kwa tuhuma za kuiba magunia mawili ya korosho kutoka kwenye eneo la ajali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la NAN, polisi waliwashtaki Hassan na Samson kwa kula njama ya uhalifu na wizi.
Hata hivyo, walikana mashtaka hayo Mwendesha mashtaka, AdamuOchone, alieleza mahakama kuwa mlalamikaji, Isah Jaru, aliripoti tukio hilo katika kituo cha
polisi cha Tuga Maje mnamo Februari 23, 2025.
Ochone alisema kuwa mlalamikaji alikuwa akiendesha pikipiki yake kwenda kununua korosho, lakini aligongwa na gari lisilojulikana karibu na mji wa Giri, Abuja, mnamo Februari 22.
Alisema kuwa mlalamikaji alikimbizwa hospitalini kwa matibabu, lakini aliporudi kwenye eneo la ajali kuchukua pikipiki yake pamoja na magunia mawili ya korosho,
aligundua kuwa havikuwepo tena.