PROF. KABUDI SUALA LA UKARABATI WA VIWANJA NI ENDELEVU
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi amesema ukarabati wa miundombinu na viwanja vya michezo nchini ni suala endelevu na shirikishi, kwakua Serikali inakaribisha wadau mbalimbali katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu hiyo.
Waziri Prof. Kabudi amesema hayo leo, Mei 19, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge kuhusu ukarabati na ujenzi wa viwanja vya michezo.
Akijibu swali la nyongeza la Mhe. Aziza Ally mbunge wa Viti Maalumu ameeleza kuwa, wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI inaandaa mpango maalumu wa kuboresha viwanja vya michezo katika shule za msingi na sekondari kwa kutoa ushauri kupitia wataalamu wa wizara.
Aidha, Serikali imetenga viwanja vitano kwa ajili ya mazoezi wakati wa michuano ya AFCON mwaka 2027 ambavyo ni uwanja wa Jamuhuri Morogoro, Mkwakwani Tanga, CCM Kirumba Mwanza, Sokoine Mbeya pamoja na Majimaji Songea.