Waislam Watashuhudia Ramadhan 2 Mwaka 2030
Waislam Watashuhudia Ramadhan 2 Mwaka 2030
Mwaka 2030, Waislamu watafunga mwezi mtukufu wa Ramadhani mara mbili. Ramadhani ya kwanza Januari, kisha tena mwishoni mwa Disemba.
Hili linatokea kutokana na tofauti kati ya kalenda ya Kiislamu ya Hijria na kalenda ya Gregori inayotumika duniani kote.
Ramadhani inafuata mzunguko wa mwezi, huku kalenda ya Gregori ikihesabu mwendo wa Dunia kuzunguka Jua. Kutokana na tofauti hi, kila baada ya miaka takriban 30, Ramadhani hujitokeza mara mbili ndani ya mwaka mmoja wa Gregori.
Mara ya mwisho ilitokea mwaka 1997, na baada ya 2030, tukio hili linatarajiwa kujirudia mwaka 2063. Vilevile, kutokana na tofauti ya kalenda hizi mbili, Ramadhani huangukia katika misimu tofauti kila baada ya miaka kadhaa.