RAIS WA GHANA MHE MAHAMA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI MKOANI ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. John Dramani Mahama amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania ambapo amekuwa Mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushiriki katika ufunguzi wa mwaka mpya wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu na sherehe za Kumbukizi ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo mwaka 2006.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA), Mhe. Mahama ameagwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi CCM na serikali.






