Sijapenda Uteuzi wa Mojtaba Khamenei
Sijapenda Uteuzi wa Mojtaba Khamenei
Rais Donald Trump wa Marekani amesema amesikitishwa na kitendo cha Iran kumteua Mojtaba Khamenei kuwa Kiongozi Mkuu wao baada ya kifo cha Baba yake akisema Mojtaba ataleta matatizo kama ya Baba yake au hata zaidi kwa Wananchi wa Iran.
Akiongea na Waandishi wa Habari Trump amesisitiza kwamba chaguo hilo la Watu wa Iran limemsikitisha sana.
Ayatollah Alli Khamenei aliuawa na Marekani wakishirikiana na Israel kwenye shambulizi walilolifanya Iran ambapo kufuatia kifo chake Iran imemteua Mtoto wake wa kiume Mojtaba kurithi mikoba ya Baba yake na jana makombora ya kwanza yamerushwa chini ya Uongozi wake.






