Zanzibar Pumzikeni Juma Tano Mwaka Mpya Wakiislam
Zanzibar Pumzikeni Juma Tano Mwaka Mpya Wakiislam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza kuwa Jumatano, Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko kwa Zanzibar ili kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa tamko hilo leo, Juni 15, 2026 Ikulu Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Serikali wa kuutambua Mwaka Mpya wa Kislamu kuwa miongoni mwa siku muhimu Zanzibar.
Amesema siku hiyo itatoa fursa kwa Wananchi, hususan waumini wa dini ya Kiislamu kuukaribisha mwaka mpya kwa ibada, dua na matendo mema pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuijaalia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla amani, umoja na ustawi.
Alhaj Dkt. Mwinyi amewataka Wananchi kuutumia mwaka mpya huo kujitathmini, kuimarisha uchamungu, kusaidiana na kuendeleza maadili mema yanayojenga familia na Taıta lenye mshıkamano.
Aidha, amezitaka Taasisi za Serikali, Taasisi Binafsi, Waajiri na Wananchi wote kuzingatia tangazo hilo kwa mujibu wa taratibu zilızowekwa.
Rais Dkt. Mwinyi amewatakia Waislamu na Wananchi wote heri ya Mwaka Mpya wa Kiislamu 1448 Hijria, akimuomba Mwenyezi Mungu aufanye kuwa mwaka wa kheri, amani, afya njema na maendeleo kwa wote.





