Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.Mwigulunchemba (Mb), amekutana na baadhi wa wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amekutana na baadhi wa wanachama wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na kuwaeleza jitihada zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na uhaba wa dola za Marekani katika mzunguko wa fedha na kuwataka kuzalisha bidhaa zililoongezwa thamani na kuziuza nje ya nchi ili kuongeza upatikanaji wa dola nchini, Mkutano huo ulioandaliwa na CTI, umefanyika katika Hoteli ya New Afrika (Four Points by Sheraton), Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuria pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.








