Kifo Cha Mohbad Ongopeni Unafki

Kuna rafiki yangu mmoja kutokea huko Tabora Kanyenye Majuzi Alinipigia simu na kuniuliza Kaka nimesikia Taarifa Nyingi kwenye mitandao wanasema eti marehemu 2pac shakur hakufariki Dunia Alikuwepo huko America Ya Kusini kwenye nchi ya Mexico 🇲🇽 Mara Cuba 🇨🇺 akiishi vizuri tu Tena wamepanga watamuonesha maisha yake yote alivyokuwa akiishi huko (movie ina kuja very soon) nilimwambia hivi uongo kuna muda unabadilika na kuwa ukweli..

Nikukumbushe tu rafiki yangu tambua kuwa kila nafsi itaonja umauti 💔 Na tambua pia kila kifo huwa kinakuwa na sababu yake hapa namkumbuka mwalimu wangu wa Kiswahili na msamiati wake wa Siri ya maiti aijuae muosha.. Nimeona watu wengi kweli kwenye mitandao kutwa wao ni kumtukana Msanii #Nairamaley pengine hata hawajui Naira alikutana vipi na #Mohbad Mpaka kumsaini kwenye lebel yake ya #marlianmusic Au pia ndio tenda wema nenda zako.

Nimeona page Nyingi huko #nigeria kinachoandikwa nisawa kabisa na ninachokisikia kutoka kwa wanamitandao wa nchi ya #Samia wakiongozwa na kaka yanga #skytanzania Lakini mmejaribu kufikiria na kuruhusu masikio yenu yasikie na upande wa pili au ndio mmeziba kabisa masikio Mpaka Punda afe mzigo Ufike.

Wakati mwingine ni kweli tunaumizwa na watu wetu wa karibu wanapotutoka Lakini ukweli hauwezi kufutika hivi mmejaribu kuwaza kuwa #mohbad alikuwa anatumia baadhi ya drugs na mara kadhaa bosi wake huyo wa zamani #nairamaley alijaribu njia Nyingi kuweza kumsaidia #mohbad hata kumpeleka soba house lakini bado watu wamekomalia Naira muuwaji sawa yawezekana amehusika kwa namna moja ama nyingine sikatai.

Lakini swali kwetu sisi ambao leo hii ndio Ndugu zake wakaribu na #mohbad kwanini hatukumsapoti kazi zake ziweze kushika charts kubwa mpaka Leo hii amekufa eti ndio ngoma zake zinatrendi na kuchezwa na kila media kama sio UNAFIKI ni Nini.

Wasanii wangapi hata hapa nyumbani wanapoteza maisha kwa sababu ya depression wanalalamika Sanaa ni ngumu au mpaka niwataje basi hata dada yangu #rubby katoka kuongea majuzi tu kuwa anapitia magumu..

Wasanii wangapi hata hapa nyumbani wanapoteza maisha kwa sababu ya depression wanalalamika Sanaa ni ngumu au mpaka niwataje basi hata dada yangu #rubby katoka kuongea majuzi tu kuwa anapitia magumu.. kinachoniuma sio #mohbad kuongelewa ila kinachoendelea sasa ni siasa na watu kucreat story wapige pesa Mara alipelekwa hospital akiwa amekufa mara tumekuta Damu kwenye kaburi mara daktari aliyemchoma ni feki.

Sasa mengine mpaka nafikiria hivi ni mimi tu ambaye nilikuwa nachomwa sindano utotoni na Wakubwa zangu na napona vizuri tu na hata sio professionalisms yao au wale ambao bahati mbaya walizaliwa wakati wakiwa majumbani mwao wale wakunga tuwafungulie kesi na wao Kuna muda huwa inafika hata uwanjani mchezaji anamwokoa mchezaji mwenzake kabla ya hao madaktari kufika.

Dunia ya sasa yeye CCTV camera karibu kila mahari bado inataka tuamini kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza ieleweke sitetei (watu) Taarifa za #mohbad kuuliwa ila UNAFIKI na mkumbo wa watu usiwafanye hata wale wasiokuwa na hatia wakaingia hatiani.

Naira amefeli wapi ?

Itaendelea……..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button