DR Congo imesema haitaongeza muda wa Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Kikosi cha Afrika Mashariki kilichoundwa ili kukabiliana na ghasia za wanamgambo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimeamriwa kuondoka baada ya kuhudumu kwa miezi 11.
Serikali ya DR Congo imesema haitaongeza muda wa Jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya miezi kadhaa ya kulalamikiwa kushindwa kupambana na kundi la waasi la M23.









