Wanajeshi watatu wa Tanzania wameuawa mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Wanajeshi watatu wa Tanzania ambao ni sehemu ya Kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, wameuawa mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kikosi hicho kilitumwa kusaidia wanajeshi wa serikali ya Kongo kupambana na waasi wa M23 ambao wamekuwa tishio kwa usalama eneo hilo. Mwanajeshi mwengine mmoja kutoka Afrika Kusini amefariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini.






