Mtanzania Kuwakilisha Vijana Wafrika Mashariki (AU)
Mtanzania Kuwakilisha Vijana Wafrika Mashariki (AU)

Mtanzania Sylviabay Kijangwa Achaguliwa
Mjumbe wa WiseYouth Katika Umoja wa Afrika Mwanadiplomasia kijana kutoka Tanzania.
Sylviabay Kijangwa, amechaguliwa kuwa mjumbe wa WiseYouth, tawi la Baraza la Wazee chini ya Baraza la Amani na
Usalama la Umoja wa Afrika. Akiwakilisha Afrika Mashariki, atachangia katika juhudi za kutatua migogoro, upatanishi na kujenga amani barani Afrika.





