Yanga Yaondoka na Alama 3 Dhidi Ya Mashujaa.
Yanga Yaondoka na Alama 3 Dhidi ya Mashujaa
Prince Dube ameonyesha makali yake
akiwa na jezi ya Yanga baada ya kutumia dakika 53 kufunga hat trick ya kwanza Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/2025, dhidi ya Mashujaa.
Dube ambaye alikuwa hajafunga bao lolote kwenye ligi msimu huu, alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza katika dakika ya nane ya mchezo, huku akitupia la pili dakika ya 23, David Ulomi alifungia Mashujaa dakika ya 45 kwa shuti kali.

Staa huyo ambaye alijiunga na Yanga akitokea Azam FC alikamilisha hat trick yake dakika ya 53 ya mchezo, hata hivyo, dakika 11 mbele Mashujaa walifunga bao la pili
kupitia kwa ldrissa Stambuli kwa shuti la mbali na mechi kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Sasa Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 30, zikiwa ni tatu nyuma ya Azam inayoongoza ligi ikiwa na pointi 33,
lakini ikiwa imecheza michezo mitatu zaidi.





