Elon Musk na Wawekezaji Wapo Tayari Kununua OpenAl
Elon Musk na Wawekezaji Wapo Tayari Kununua OpenAl
Mwekezaji bilionea ElonMusk, kwa kushirikiana na kundi la wawekezaji akiwemo Vy Capital, kampuni yake ya Al (XAI), na mfanyabiashara wa Hollywood Ari Emanuel, wamewasilisha dau la dola bilioni 97.4 kununua OpenAI.
Hatua hii imechochea mvutano wa muda mrefu kati ya Elon Musk na Mkurugenzi Mtendaji wa 0penAl, Sam Altman.
OpenAl kwa sasa iko kwenye mazungumzo ya mwisho ya kupata ufadhili wa dola bilioni 40 kutoka SoftBank, ukikadiria thamani yake kufikia dola bilioni 300.
Ingawa OpenAl haijatoa jibu rasmi kuhusu kuuza, Altman alijibu kwa utani kupitia mtandao wa X, akisema, “Hapana asante, lakini tuko tayari kununua Twitter kwa dola bilioni 9.74 kama unataka.” Musk alijibu kwa kumuita Altman “tapeli, hali inayoongeza mvutano kati yao.
Wachambuzi wa masoko wanaamini kuna uwezekano wa 10% kwamba Musk ataweza kuinunua OpenAI kufikia mwaka 2025. Ikiwa atafanikiwa, wawekezaji walioweka dau la “ndiyo” wanaweza kupata faida mara 10 ya
uwekezaji wao, huku wale walioweka dau la “hapana’ wakitarajiwa kupata faida ya 11%.






