Watanzania Mtusamehe kama Tumewakosea.

Watanzania Mtusamehe kama Tumewakosea

Rais wa Kenya, William Ruto amewaomba msamaha Watanzania kama kuna jambo lolote ambalo Kenya imeikosea Tanzania. Akiongea wakati wa maombi maalum ya kuliombea Taifa la Kenya leo May 28,2025, Ruto amesema

“Nimesimama hapa kuwaambia kwamba nina uhakika na kesho bora ya Kenya na sina wasiwasi najiamini kwamba Kenya ni nchi iliyobarikiwa na kesho ya Kenya haijalishi kitu gani kimetokea itakuwa nzuri ”

“Majirani zetu kutoka Tanzania kama kuna kitu tumewakosea kwa namna yoyote, mtusamehe, Rafki zetu wa Uganda kama kuna kitu tumefanya ambacho hakipo sawa tunaomba radhi, kwa Watoto Wetu (ikiwemo Gen Z) kama kuna hatua zozote mbaya mmefanyiwa tunaomba radhi, kwa Majirani zetu kama kuna hatua yoyote tumefanya mtusamehe, tunataka kujenga ushirikiano ambao utaifanya nchi yetu kuwa bora”

Ruto ameomba radhi wakati huu ambapo kumekuwa na malumbano makubwa mitandaoni kati ya Wakenya na Watanzania tangu Mwanaharakati Martha Karua na wenzake waliporejeshwa nchini kwao baada ya kuwasili Tanzania kufuatilia kesi ya Tundu Lissu ambapo malumbano hayo yameshika kasi zaidi baada ya Wabunge wa Mabunge ya nchi zote mbili kutoa maoni yao tofautitofauti kuhusu kinachoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button