Waziri Mkuu Ajiuzuru Kisa Wananchi Kulalamikia Bata la Mtoto Wake
Waziri Mkuu Ajiuzuru Kisa Wananchi Kulalamikia Bata la Mtoto Wake.
Waziri Mkuu wa Mongolia, Oyun-Erdene, amejiuzulu kufuatia maandamano makubwa yaliyozuka baada ya mtindo wa maisha ya kifahari wa mwanawe kuonekana kwenye mitandao ya kijamii.
Mwanawe alionyesha begi la Dior na mifuko kadhaa ya manunuzi alipokuwa kwenye likizo ya uchumba.
Picha ya begi la Dior, inaripotiwa kupostiwa na mchumba wake, ilikuwa na maelezo yaliyosomeka: “Happy birthday to me” (Heri ya siku yangu ya kuzaliwa). Picha nyingine ilionyesha wanandoa hao wakibusiana wakiwa katika swimming pool.
Luvsannamsrain Oyun-Erdene, ambaye amekana kufanya kosa lolote, alipoteza kura ya imani bungeni siku ya Jumanne.







