Bado Siku 5 Ijulikane Mwenye Nguvu ya Soka ni Yanga, Simba au TFF
Bado Siku 5 Ijulikane Mwenye Nguvu Ya Soka ni Yanga,Simba au TFF?
Mapacha wa Kariakoo bado wanaendelea kutunishana misuli wakitaka kuonyesha kwenye Jamii kuwa wao ndio wanaliendesha soka la Tanzania.
Yanga kaweka msimamo hachezi mpaka baadhi ya watu wajiuzulu kwenyw nafasi zao hasa Bodi ya ligi Tanzania kama halijafanyika hilo HAWACHEZI NG’OO.
Simba wanasisitiza kuwa waliowafanyia vurugu wakati wanaenda mazoezi wachukuliwe hatua za Kisheria ila Tarehe 15 wanaleta timu Uwanjani na wanacheza.
Simba mechi ya kwanza waligomea wakataka wahuni wote hasa mabodigadi wa Yanga wachukuliwe sheria na waliowazuia kuingia Uwanja.
Licha ya kuwa bado hakuna aliyechukuliwa sheria wamekubali kuirudisha timu Uwanjani huenda wamejiridhisha na maelezo ya TFF.
Yanga wanasema Hakuna wa kuikata Pointi na Wanajiondoa lwenyw ligi endapo malalamiko yao hayajachukuliwa sheria.
TFF wao wanasema mchezo upo hiyo Tarehe 15 na taratibu zote zipo pale pale. Kama Yanga hawataleta timu wanatakiwa kupokonywa alama tatu na magoli matatu lakini pia kupokonywa alama ambazo zipo kisheria au kushushwa daraja.
Swali liilopo na kitu ambacho wengi wanasubiria kuona ni je TFF watachukua hatua stahiki kwa mwenyw makosa au ubinadamu utatumika??





