Tyrese amefanya Surprise kwa kumtembelea Baba yake nyumbani kwake St. Louis, Kwa mujibu wa Tyrese, Baba yake amekuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kansa
Mwigizaji maarufu Tyrese Gibson, anayefahamika zaidi kwa kuigiza kama “Roman Pearce” kwenye mfululizo wa filamu za “Fast & Furious”, leo ameonesha upendo wa kipekee kwa Baba yake mzazi katika kuadhimisha Siku ya Baba Duniani (Father’s Day). Tyrese amefanya #Surprise kwa kumtembelea Baba yake nyumbani kwake St. Louis, akiwa ameambatana na zawadi mbalimbali zenye ishara ya upendo na shukrani.
Kwa mujibu wa Tyrese, Baba yake amekuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kansa, ambao kwa sasa umefikia hatua ya nne (Stage 4) na umemuathiri sana kiafya. Hata hivyo, Tyrese ameandika kuwa leo akiwa na Baba yake wametumia muda wao pamoja kupiga stori, kucheka, kula na kufurahi.
Vipi kwa upande wako, leo katika maadhimisho haya ya Siku ya Baba Duniani, umeitumiaje siku hii kumkumbuka au kumuonesha upendo Baba yako?






