Serikali Yakiri Kuwashikilia Vijana Hawa Wa Arusha.
Serikali Yakiri Kuwashikilia Vijana Hawa Wa Chadema Arusha.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupitia kwa Kamanda wake Justine Masejo, limethibitisha kuwakamata na kuwashikilia Vijana wawili ambao ni Jackson Lubalo na Josephn Mrindoko wa Kundi la Mtandaoni la Wachokonozi.
Akiongea kwa ufupi kwa njia ya simu, Kamanda Masejo amethibitisha kukamatwa kwa wawili hao na kusema uchunguzi utakapokamilika Jeshi la Polisi litatoa taarifa kamili.
Jeshi hilo limethibitisha haya ikiwa ni saa kadhaa tangu Mwenyekiti wa Kijiji cha Maji ya Chai Wilayani Arumeru Mkoani Arusha Mase Mbise akiri kuwa Ofisi yake ilipewa taarifa na Polisi juu ya kukamatwa kwa mmoja wa Vijana hao ambaye ni Joseph Mrindoko na kueleza kuwa Polisi walianzia kutoa taarifa Ofisi ya Kijiji kuhusu ukamataji huo.
Mbise alieleza kuwa baada ya kumkamata Kijana huyo akiwa kwenye gari dogo akiwa na Mtu mwingine anayetajwa kuwa Fundi, walikwenda nyumbani kwake na kufanya uchunguzi pamoja na kuchukua vitu mbalimbali ikiwemo kinasa sauti, camera stand ya camera, vitabu vyake na kuviandikisha chini ya uongozi wa Serikali ya Kijiji.





