Tulia Achukuliwa Form ya Ubunge na Wananchi wa Uyole
Tulia Achukuliwa Form ya Kugomea Ubunge na Wananchi wa Uyole
Aliyekua Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson amekabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo la Uyole, aliyochukuliwa mapema hii leo na wananchi wa jimbo hilo.
Wakimkabidhi fomu hiyo wananchi wa jimbo la Uyole wameeleza lengo la kumchukulia fomu Dkt. Tulia ikiwa ni kuunga mkono jitihada zake katika kuwahudumia wananchi na kumtaka aijaze na kuirejesha kwa wakati.






