Usiri wa Vipato kwa Wanandoa Chanzo cha Upotevu wa Mali
Usiri wa Vipato kwa Wanandoa Chanzo cha Upotevu wa Mali
Mhariri Mbunifu wa Video wa Kampuni ya Mwananchi, Geofrey Mlwilo amesema usiri wa vipato miongoni mwa wanandoa ni chanzo cha mali kupotea bila mpangilio.
Hayo amesema leo Jumatano, Julai 16, 2025, wakati akichangia mjadala wa Space ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ukiwa na mada isemayo: Je, ni muhimu kwa wanandoa kuelezana ukweli wa vipato vyao halisi ili kuimarisha uchumi wa familia?.”
“Kuna umuhimu mkubwa wa kuelezana ukweli wa vipato, ingawa kuna mmoja kati yao anaweza kujitokeza akawa na wasiwasi ikiwa mbele ya safari wataachana. Lakini kuelezana ukweli ni ulinzi mzuri wa mali za familia,” amesema.

Kwa mujibu wa Geofrey kuelezana ukweli kunajenga uaminifu, hivyo ukweli kuhusu vipato huondoa mashaka na hofu kati ya wanandoa na huimarisha uaminifu ambao ni nguzo ya ndoa bora.





